STORY:BABA NTILIE MGANE 33,34 na 35

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 33
Inaendeleaaa»»»»»»»»»»»»»
Baada ya mama yao kumaliza kuosha vyombo akaketi sofani jackline akaamua kuvunja ukimya na kuuliza *mama huyu nani?*
*Huyu ni dada yenu mtakuwa mnashinda nae hapa nyumbani kuanzia leo*alitambulisha mama yao
*Karibu dada,anaitwa dada nani?*aliuliza Jackson
*Asante*alijibu yule dada
*Anaitwa dada zawadi?*alijibu mama yao
*Karibu sana dada zawadi*alimkaribisha jackline
*Asante sana wadogo zangu* alijibu zawadi kwa furaha
Zawadi alikuwa binti mzuri sana na alimzidi mama wawili kwa uzuri alikamilika kila idara,usiku baba wawili aliporudi aliwakuta wameketi wakiangalia filamu baada ya kumaliza kula chakula cha usiku wakati huo zawadi alikuwa chumbani kwake kajipumzisha zawadi,aliita mama wawili
*Abee mama* aliitika zawadi akaja sebuleni shikamoo alisalimu
Marahaba haujambo,aliitikia baba wawili
Sijambo,alijibu
*Zawadi huyu ni baba yako yaani mume wangu mimi* aliongea mama wawili
*Keti hapa sofani kwanza* aliongea mama wawili na zawadi akaketi
*Mume wangu huyu ndio yule msichana niliyekwambia nitamleta ili awe anashinda na watoto anaitwa zawadi* alitambulisha mama wawili
*Oooh sawa,karibu sana zawadi*alimkaribisha baba wawili
*asante sana baba* alijibu zawadi
*Nashukuru kukufahamu baba na nafurahi kukuona* aliongea zawadi huku akirembua jicho lake na lilivyokubwa likawa kama linataka kudondoka au kabanwa na usingizi lakini mama wawili hakuona hilo tukio
* Haya kaendelee na kazi zako* alisema mama wawili
* Haya usiku mwema* aliongea zawadi na kuelekea chumbani kulala
*mmh* aliguna baba wawili
*Unaguna nini mume wangu* aliuliza mama wawili
*Hamna kitu mke wangu nakupenda sana hakuna kama wewe na hatotokea* aliongea baba wawili ila moyoni aliona mkewe kajipalia makaa ya moto maana yule si msichana wa kazi ila anataka awe mke lakini hakutaka mkewe ajue
*Sawa mume wangu nami nqkupenda pia*,alijibu mama wawili walinyanyuka na kwenda kulala
Kesho yake saa 11:30 alfajiru zawadi aliamka kukiwa bado giza akawasha taa akaanza kufanya usafi huku akivalia vazi la khanga na nguo ya ndani tu hivyo umbo lake lilionekana kama lilivyo tabu ni akiinama hadi nguo ya ndani inaonekana. Aliamka mama wawili na kumkuta kainama *eeh wewe ndio nini kutumwagia radhi kiasi hicho na hilo vazi gani?* aliuliza kwa mshangao
*Abee ni....meona hakuna mtu mama* alijibu zawadi kwa woga maana lengo lake ni yule baba amtamani sio akutwe na mama wawili
*Ata kama hamna mtu ndio vazi la kuvaa hilo?mmh wewe* aliuliza na kuguna
*Nisamehe mama* alijibu zawadi
* Kavae nguo haraka* aliamuru mama wawili
*Sawa mama* alitoka akaenda kuvaa gauni akarudi kuendelea na usafi
*Hapo sawa sio unakuwa hauheshimu mwili wako sawa hapa marufuku kuvaa na kukaa mikao ya ajabu* alitoa onyo mama wawili huku akimuangalia
*Sawa mama haitojirudia tena* alikubali amri ile zawadi
Alipomaliza usafi aliandaa kifungua kinywa wakati huo mama wawili aliinjika maji ya kuoga mumewe yalipopata moto alimimina kwenye ndoo akayapooza akaingia nayo chumbani kwake akamuamsha mumewe,aliamka akaoga akatoka mama wawili nae akaenda kuoga akaoga alipomaliza wakatoka mpaka meza ya chakula wakanywa kifungua kinywa walipomaliza wakaondoka kuelekea kazini.
Watoto waliamka saa 2:30 asubuhi wakaoga nakuswaki alafu wakanywa chai wakamshukuru dada yao,akatoa vyombo akaviosha na kuvipanga kabatini,watoto akawawashia runinga wakawa wanaangalia kipindi cha katuni,saa tano kasoro alitoka akafungua mlango na kumuingiza  mkaka mmoja mweusi tii mrefu akampeleka mpaka chumbani kwake,watoto wakawa wanashangaa mara wakasikia kelele tu wasijue nini kinaendekea baadaye walitoka yule mkaka akaondoka ilikuwa imetimia saa sita mchana,zawadi akaanza kupika alimaliza saa saba mchana akaenda kuoga akabadili nguo ndipo akapakua chakula ila aliwapa onyo wale watoto (ole wenu mje mumuambie mama kama kuna mtu aliingia chumbani kwangu nitawakomesha) wakawa wanamuogopa ,mama yao alirudi akala akaingia chumbani kupumzika.
Watoto hawakuwa na amani ata kidogo walimuogopa sana dada yao kila alipokuwa anawaangalia waliangalia chini baadaye wakaamua kwenda kulala wakamuacha peke yake pale sebuleni saa 12:30 baba wawili alirudi akamkuta zawadi sebuleni shikamoo baba alisalimia huku akinyanyuka kumpokea begi akaidondosha khanga makusudi akabaki na nguo ya ndani tu lengo lake kumteka baba wawili *wewe vaa nguo yako* aliongea baba wawili na kumpita aliokota khanga kwa aibu kubwa maana akadhani kama anaweza akaniambiwa hivyo na mwanaume rijali yoyote hivyo akahisi jogoo hapandi mtungi,mama wawili aliamka akaenda kupika chakula alipomaliza akawaamsha watoto wakala,mama wawili hakutaka kumpa upenyo yule msichana wa kazi kumhudumia mumewe chochote zaidi ya chai.

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 34
Inaendelea»»»»»»»»»»»»»»»
Kwanini mama kazi hauniacha mimi zote kama kufua nguo zako na za baba?,alimuuliza swali mama wawili
Hapa ndipo wanawake wengi wanafeli unakuta mwanamke ameolewa anamhudumia mumewe vizuri kila kitu ila akitafuta mfanyakazi wa ndani tu anamuachia majukumu yote hadi kufua nguo za ndani za mumewe anakua anafua dada wa kazi,sasa siku msichana wakazi akimfumania na mumewe anaanza kumlaumu mumewe anasahau chanzo cha tatizo ni yeye kujisaulisha wajibu wake kama mke na siwezi kukuachia ufue nguo za mume wangu labda mimi nife,aliongea mama wawili
Mmh ukiumwa je? Aliuliza zawadi huku akiona lengo lake kuolewa na yule baba limekufa
Labda nilazwe na ata nikilazwa atakuja wifi yangu kufua sio wewe mtu baki,aliongea mama wawili kwa kujiamini
Eeh haya mama,alijibu zawadi huku pozi likimuisha
Likizo ikiisha na watoto walirudi shule,mama yao aliwaambia elimu ndio kila kitu kwao ila wasisahau kumtanguliza Mungu katika kila jambo waliombalo na walifanyalo maana yeye ndio kila kitu kwao na pasipo yeye hawawezi kufanya chochote,walikubali na kumuahidi hawatasahau kamwe.
Kuna siku baba wawili alisahau simu yake nyumbani hivyo alirudi kuichukua alipofika alimkuta zawadi sebuleni shikamoo baba alisalimia zawadi akinyanyuka akasogea mpaka alipo baba wawili akambusu mdomoni.
Umemaliza au? Aliuliza baba wawili mara baada ya zawadi kutoa mdomo wake aliokuwa ameukutanisha na mume wa bosi
Hamna unajua nini mwenzio nawashwa nahitaji kukunwa tafadhali nisaidie nakuomba,aliongea zawadi huku akimlemba sauti na kurembua jicho lake
Baba wawili hakuongea akaingia chumbani kwao ambapo zawadi alimfata akaanza kumpapasa bila mpangilio kana kwamba kapandwa na wazimu,alimuangalia akamuambia jaribu kuwa na heshima siwezi kulala na wewe bado haujajua kuoga kama mke wangu na wewe sio mzuri ila ni mbaya kuliko mtu yoyote hapa duniani unajiona mzuri kwakuwa unadanganywa ebu kajiangalie kwenye kioo afu kikadilie ukizaa itakuaje,akachukua simu yake akamsukumia zawadi nje akafunga mlango na kuondoka huku akimuacha zawadi kasimama kama mlingoti
*Mmh hivi ananionaje huyu eti mimi sio mzuri huyu kipofu si bure zawadi mimi na mkewe nani mzuri kwanza mkewe kakomaa kama mawe ya mwanza,afu eti sijui kuogq asiyejua kuoga mkewe sio mimi najua kuoga sana ndio maanq wanaume wengi wananipenda na wote wanataka kunioa huyu mbaba hajielewi yaani anakataa bahati daah kalogwa huyu* aliongea zawadi peke yake
Baba wawili alipofika ofisini kwake alimtumia mkewe ujumbe na kumwambia kila kitu,kuanzia siku ya kwanza mpaka kituko alichofanyiwa siku hiyo mkewe alishtuka sana akamwambia usijali nitamkanya,alimjibu mama wawili kiti alichokikalia kiliwaka moto akasimama miguu inamwambia mfate tu akamuaga mfanyakazi wake akabeba mkoba wake akarudi nyumbani alipofika alimkuta zawadi sebuleni shikamoo mama,alisalimia zawadi
Marahaba haujambo,aluuliza mama wawili
Sijambo,alijibu zawadi
Umeshindaje?, aliuliza akizunguka pale sebuleni
Salama mbona unazunguka kuna nini mama?,aiuliza zawadi bila kujua tatizo ni yeye
*Zawadi* aliita mama wawili
*Abee mama* aliitika zawadi
Akaketi kwenye sofa njoo uketi hapa nilipo,aliongea mama wawili zawadi akukataa wala kupingana na kauli ya bosi wake huyu akakaa karibu kabisa
*Mimi ni nani yako?* aliuliza mama wawili huku akimtazama zawadi usoni
*Mama yangu* alijibu zawadi
*Oooh unaweza kulala na baba yako mzazi?* aliuliza mama wawili
*Hapana siwezi* alijibu zawadi kwa kujiamini sana uku kengele za hatari zikigonga kichwani mwake
*Jibu zuri sana,kwanini unajidharau na kujidhalilisha?* aliuliza mama wawili
*Najidharau kivipi mama na najidhalilishaje?* aliuliza akijifanya haelewi hapo akili yake ikamwambia umeumbuka kila kitu kiko wazi
*Wewe ni mtoto wa kike sharti ujiheshimu ili Mungu akupe mume mwema wa maisha yako sio kujidhalilisha kwa wame za watu  tena wasio na malengo wala muda na wewe,je unamtaka baba yako?* aliuliza baada ya ushauri mzuri na mfupi
*Hapana mama* alijibu zawadi huku akikosa amani kabisa moyoni mwake
*Unataka akuchezee au? Unajua wanaume ni viumbe wa ajabu sana anauwezo akalala na wewe ili akidhi haja zake za muda mfupi na mwingine anaweza akalala na wewe kwakuwa umemtaka na si kwamba anakupenda ila anataka kukufunua tu na si mume wangu ni wanaume wote* aliongea wawili
*Sawa mama nimekuelewa* aliongea zawadi kwa unyonge sana
Usijali mdogo wangu jirekebishe,aliongea mama wawili

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 35
Inaendeleaa»»»»»»»»»»»»»»
Kingine swala la kuingiza wanaume humu ndani si kwamba sijui nalijua ila nilitaka siku moja niongee na wewe kwa kina ili nijue tatizo kubwa nini,aliongea mama wawili
*Nisamehe mama sirudii tena* aliongea zawadi machozi yakimdondoka
*Sawa ila kujirekebisha ni wewe sitoongea tena* alisema mama wawili na maongezi mengine yakaendelea. Kuanzia hapo zawadi alimheshimu sana baba wawili na mama wawili kupita mawlezo kwakuwa lengo la mama wawili ni kumfanya zawadi asimame kwa miguu yake alimpeleka chuo akasomee kozi ya kutoa ushauri alipohitimu akamfungulia ofisi na kumpangia chumba alimlipia mwaka mzima mkataba wao ukawa umeishia hapo
Mama wawili na mumewe waliongeza masaluni na maduka na sasa walifungua mikoa mbalimbali huku watoto wao wakizidi kusoma kwa bidii,baada ya anna kukaa peke yake bila mwanaume au mume kwa muda mrefu hatimaye alipata mwanaume wa kumuoa ambae alikuwa ni mafrika kusini hivyo ndoa ilifungwa kanisani anna na mumewe waliondoka na kwenda kuishi afrika kusini baada ya miaka miwili anna alibahatika kupata mtoto wa kike aliyempa jina la malaika.
Jackline alisoma kwa bidii na kufanikiwa kumaliza elimu yake vizuri ya udaktari hivyo akaajiriwa kuwa daktari bingwa wa magonjwa ya moyo nchini marekani,kaka yake nae aliajiriwa nchini china kama fundi mitambo aliyebobea,babu yao alifurahia sana mafanikio ya wajukuu zake na kila siku aliwaombea wafanikiwe zaidi. Umri wa mzee Raphael ulizidi kusogea nguvu nazo zikamwishia alifikia hatua ya kujisaidia kila kitu hapohapo,mama wawili aliapa kumhudumia mpaka mwisho,alimuuguza mkwewe bila kinyaa chochote ingawa watu walimcheka wala hakujali kuhusu hilo aliendelea kufanya kama alivyouahidi moyo wake na katu akukata tamaa,mzee raphael aliandika mali zake zote jina la mkwewe kutokana na kumjali na kumthamini kwa kipindi kigumu anachopitia tofauti na anna ambae alikataa kurudi kwa madai mumewe amemkatalia,majira ya saa 8:00 usiku mbala mwezi iliangaza mfano wa jua kali la saa sita mzee raphael alimkabidhi mkwewe hati zote akamwambia hii ni mali yako na shukrani yangu kwako,naomba niletee biblia mama yangu alinyanyuka akaenda kumletea alisoma neno alipomaljza akaimba pambio la kusifu ile anamaliza kuimba akafumba macho,mwezi na nyota vikafunikwa na giza nene,baba baba amka baba aliita mama wawili lakini akuitika
Akapiga simu kwa mumewe akuongea zaidi ya kulia tu akakata akampigia Anna huku akilia*,kuna nini?* Anna aliuliza kilio kilizidi kwa wifi yake akakata simu na kumpigia kaka yake simu haikupokelewa akatuma ujumbe haukujibiwa akaanza kulia na kumwambia mumewe baba yake amefariki alimpa pole. Mama wawili akawatumia wanae ujumbe alilia sana watu wakaja usiku huo huo mwili wa mzee Raphael ukaoelekwa hospitali waliupima wakathibitisha ameishafariki hivyo mwili ukahifadhiwa chumba cha kuhifadhia maiti,baba wawili alifika hospitali akaambiwa hali halisi akuamini alichokisikia akaenda mpaka mochwari akathibitisha kifo cha baba yake alilia sana,walirudi nyumbani watu wakaenda kulala majumbani na kuwaacha baba wawili na mkewe kulipokucha mama wawili alipeleka hati kwake mbezi maana aliambiwa asithubutu kumpa mtu yoyote hati zile ikabidi afanye alivyoambiwa akarudi tena msibani alilia sana kila alipokumbuka pambio walilokuwa wanaimba na marehemu mkwewe,mumewe akuamini japo mzigo wote alimuachia mkewe ndani ya mwaka na miezi kumi ambayo baba yao alikuwa hajiwezi kwa lolote mkewe aliubeba msalaba huo na mpaka kufariki kafia mikononi mwa mkewe sio kwake wala Anna aliumia sana.
Wajukuu zake walifika pamoja na shangazi yao Anna nao walilia sana wakati huo malaika alikuwa bado mdogo hivyo akuelewa walienda kumpumzisha mzee Raphael Jonathan maarufu kama baba ntilie kwenye nyumba yake ya milele ambapo mrithi wa mali za marehemu alitajwa kuwa ni judith yaani mama wawili watu walianza kushangaa bila kuelewa mumewe alimkumbatia akamwambia pole sana mke wangu
Asa............ nte mu.......me wa.....ngu,alijibu mama wawili akizidi kulia
Pole wifi yangu na asante kwa kumuguza baba,aliongea anna
Hakuweza kujibu alilia tu,hakika kila nafsi itaonja mauti na thamani ya mtu si kitu bali utu wake hongera sana mama wawili laiti kama wanawake wote duniani wangekuwa na moyo kama wako basi ndoa zisingekuwa zinavunjika ila tatizo wanawake wengi akiolewa anajua ndugu yake ni mumewe tu,aliongea mbaba mmoja wa makamo
Wanawake muwe mfano wa kuimarisha upendo,amani na furaha pale mnapoolewa kama alivyokuwa mama wawili yeye alikuwa kiungo cha familia yake kama ilivyo majani na maji hauwezi yanywa pekee bila sukari,aliongea zawadi
Wakarudi nyumbani muda wote mama wawili alikuwa akilia tu hadi nguvu zikamuishia baada ya msiba kuisha jackline, jackson na shangazi yao walirudi kwenye nchi zao,mama wawili akaendeleza biashara za marehemu mkwewe mpaka zikakua zaidi na utajiri wao ukaongezeka mara dufu.
           MWISHO
Upendo wa kweli hautokani na uzuri wa umbo,sura au mwendo wa mtu bali roho ya utu aliyonayo mtu,kujali,kuheshimu na kuthamini wengine.y

No comments:

Post a Comment