STORY:BABA NTILIE MGANE SEHEMU YA 29 na 30

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 29
Inaendeleaaa......
Alikuta watu wengi sana nyumbani kwao ambapo aliingia ndani akaweka mkoba wake akaanza kumtafuta wifi yake alipo wakati akiendelea kumtafuta ghafla alitokea wifi yake mbele anna wazazi wangu wameenda sitowaona tena mimi,nitawapata wapi wazazi wengine mimi ee Mungu mbona umewachukua mapema yote hii,aliongea mama wawili huku kamkumbatia wifi yake wote wakaanza kulia anna alimkumbuka mama yake alivyowaacha peke yao tena wakiwa wadogo sana alilia sana hasa ukizingatia upweke atakaokuwa nao wifi yako na pengine kubwa halilolipata wifi yake kipenzi
Siku iliyofuata taratibu za mazishi zilifanyika watu waliaga miili ya marehemu bila kuona sura zao maana majeneza yao yalifungwa,waliaga walipomaliza wakarudi nyumbani kwa mzee raphael kiukweli upweke mkubwa ulitawala ns muda wote huo mama wawili analia picha ya wazazi wake ilizidi.kumrudia kichwani mwake anna alimliwaza wifi yake na muda wote alikuwa karibu nae.
Maisha ya amani,furaha kwa mama wawili yalibadilika kabisa na ukumbuke muda huo wanae walikuwa hawafahamu chochote kuhusu msiba huo,baada ya miezi mitano kupita mapacha hawa walifunga shule wakarudi likizo na wakati huo anna alikuwa karudi arusha na babu yao mzee raphael walikuwa wanaendelea na biashara zao pamoja na baba yao alikuwa dukani kwake huku mama yao akiwa nyumbani,walifika wakagonga mlango ngongongo
Karibu aliitikia mama yao aliyekuwa sebuleni alinyanyuka akafungua mlango waoo wanangu karibuni sana jamani,aliongea mama yao akiwakumbatia
Waoo mama nao walisema wakamkumbatia mama yao kwa furaha kubwa kutokana na kutomuona muda mrefu
Karibuni ndani wanangu,alisema mama yao akawapokea mabegi akaingizwa vyumbani mwao wakaketi sebuleni na baada ya dakika tano mama yao akarudi sebuleni
Poleni na safari watoto wangu,aliongea mama yao baada ya kuketi
Asante mama tumeishapoa ila tupeleke kwa bibi na babu tukawasalimie,alisema jackline alionyesha kuchoka sana na safari sana
Mtaenda kuwaona ila subirini nitawapeleka kw babu yenu mzaa baba yenu atawapeleka  yeye huko,aliongea mama yao
Twende sasa hivi mama tumewakumbuka sana,alisema jackson
Tutaenda saa 10 jioni muda huu babu yenu yuko kazini,muda huo ilikuwa ni saa 6 mchana,aliongea mama yao
Sawa mama ngoja nikaoge nipumzike kidogo,alisema jackline
Sasa si ule kwanza,aliongea mama yake
Hapana mama,alijibu jackline akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake akalala jackline ni mbovu sana wa usingizi hivyo alivyojilaza tu usingizi ulimpitia muda ule ule,jackson mwanangu vipi habari za shule?,aliuliza mama yake
Nzuri tu mama sijui za hapa?,alijibu jackson
Nzuri tu chakula tayari karibu mezani,aliongea mama yake
Sawa mama asante sana,alijibu akanyanyuka na mama yake akanyanyuka wakaelekea meza ya chakula wakaketi mama yake akampakulia chakula nae akapakua wakala walipomaliza akaosha vyombo akarudi sebuleni wakaketi na ilipofika saa 8:30 mchana mama yao alinyanyuka akaenda kumuamsha baada ya muda mfupi jackline aliamka akaoga alipomaliza akaenda sebuleni akaketi kwenye meza ya chakula  akapakua chakula akala alipomaliza akaosha chombo akaelekea sebuleni akakaa na mama yake na kaka yake,kaka yake alinyanyuka akaenda kuoga alipotoka akamwambia mama yake tupeleke sasa
Sawa subiri nijiandae aliingia chumbani kwake akaoga alipomaliza akatoka wakaondoka kuelekea kwa babu yao mzaa baba yao ilichukua lisaa limoja  na nusu usiku wakawa wamefika kwenye safari yao
Waligonga mlango ngongo
Karibu,aliitikia mfanyakazi wa ndani wa mzee Raphael

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 30
Inaendeleaa.......
Waooo dada tulikukumbuka sana,waliongea Jackline na Jackson huku wakimkumbatia dada yao wa kazi wa babu yao.
Wao niliwakumbuka pia jamani nae aliongea kwa furaha aliwakaribisha ndani mama shikamoo alimsalimia mama wawili huku akimpokea mkoba alioubeba
Marahaba haujambo? Alijibu mama wawili na kuhitaji kujua hali ya mdogo wake huyu
Sijambo karibu sana,waliingia ndani wakaketi sofani,yule dada wa kazi alitoka akaelekea koridoni alitembea mpaka mlango wa chumbani kwa mzee raphael akagonga mlango ngongongo
Nani?,aliuliza mzee raphael
Ni mimi baba,alijibu yule dada wa kazi kwa uoga kutokana na sheria ya mzee raphael kuwa akilala hataki kuamshwa
Kuna nini?,aliuliza kwa ukali
Kuna wageni baba,alijibu huku akitetemeka
Wageni! wakina nani?,aliuliza mzee raphael
Mama wawili na wanawe,alijibu josephina kwa uoga zaidi
Waambie nakuja,alijibu mzee raphael
Josephina akaelekea sebuleni lakini kwa uoga aliokuwa ameupata haja ndogo ili mpata akaenda msalani,alipomaliza haja yake akarudi sebuleni na kumwambia anakuja
Sawa,alijibu mama wawili
Baada ya dakika tano mzee Raphael alitoka chumbani alipofika sebuleni wajukuu zake walisimama na kumkumbatia wawo babu shikamoo babu
Marahaba hamjambo,aliitikia salamu mzee Raphael
Hatujambo babu,wakamjibu akaketi nao kwenye sofa moja huku akifurahi sana,josephina
Abee baba,aliitika josephina akaja sebuleni
Waandalie wageni chakula,aliagiza mzee raphael
Sawa baba,josephina alienda jikoni akapasha mboga akawaandalia kwenye meza ya chakula akawakaribisha chakula,walikula walipomaliza akatoa vyombo akaviosha wakarudi sebuleni wakaketi.
Asante kwa kuniletea wajukuu zangu,aliongea mzee raphael
Usijali baba wamenisumbua walipofika tu wakataka waje wakuone nikaona niwalete,aliongea mama wawili
Kweli babu ila tunataka tukamuone babu mwingine na bibi,aliongea jackline
Waliangaliana mama wawili na mkwewe,sawa nitawapeleka kesho leo inabidi mlale hapa,aliongea mzee Raphael
Kweli babu?,aliuliza Jackson
Ndio nitawapeleka msijali,alijibu mzee Raphael
Kwakuwa muda ulikuwa umekwenda wakaaga *mama babu tunaomba tukalale* aliongea jackline
*Sawa nendeni wajukuu zangu* alijibu babu yao
*Josephina* aliita mama wawili
Abee mama,aliitika josephina
Wapeleke kulala usisahau kuwashushia neti,aliongea mama wawili
*Sawa mama* alijibu,akaondoka nao huku nyuma maongezi yakaendelea Tutafanyaje sasa mwanangu na ukweli unaujua bibi yao na babu yao wamefariki,je itakuwaje? aliuliza mzee Raphael
Ata sielewi baba ndio nimetaka waje hapa ili tujue tunafanyaje?,aliongea mama wawili mara mlango ukagongwa kwa kuwa ulikuwa wazi wakamwambia apite aliingia baba wawili shikamoo baba
Marahaba umekuja wakati sahihi sana,aliongea mzee Raphael
Wakati sahihi kivipi?aliuliza baba wawili
Wanao wamerudi likizo ila wanataka kuwaona babu yao na bibi yao sasa tunafanyaje? Je tuwaambie kuwa wamefariki?,aliuliza mzee Raphael
Eeh itabidi tuwaambie lakini tutaanzaje?,aliongea baba wawili na kuuliza swali
Itabidi tuwapeleke kwenye makaburi na huko tutawaambia ukweli wote baada ya kuona makaburi,aliongea mzee Raphael
Ni kweli baba bila hivyo watatusumbua sana,aliongea mama wawili
Sawa kesho asubuhi na mapema tuwapeleke na uko wataujua ukweli wote,aliongea mzee Raphael
Walikubaliana wakenda kulala.

No comments:

Post a Comment