STORY:BABA NTILIE MGANE 26,27 na 28

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 27
Inaendeleeeaaaa....
Upendo wa asha kwa mumewe ulipungua kabisa yote kutokana na kutokuwa na kazi yoyote na hivyo kumtegemea yeye ndio amlishe na kumvisha, Mariamu alikuwa bize na biashara yake tu mpaka akafanikiwa kufungua duka lingine kubwa zaidi mkoani Arusha alimfata baba yake akamuelekeza maisha yake ya ndoa jinsi yalivyo na uwepo wa mke mwenzie nyumbani,mke mwenzie huyo aliyetumia muda mwingi kumfumbia mafumbo mpaka akawa anapata hasira anatamani kupigana nae lakini yule sio mwenye makosa.
Kwahiyo wewe umeamuaje mpaka sasa na kwanini haukuniambia toka mwanzo?,aliuliza baba yake
Kiukweli baba mpaka sasa nina uamuzi mmoja tu wa kupangisha ile nyumba alafu mimi nikaishi Arusha na kama itatokea anakuja kunitafuta mwambie sipo niko nje ya nchi nahitaji kuwa huru kimawazo na kifikra,aliongea mariamu
Sawa Arusha unaenda kwa nani maana hatuna ndugu kule?,aliuliza baba yake
Bila kukuficha baba mimi kule nimefungua duka lingine kubwa la nguo za watoto na watu wazima na pia nimenunua nyumba nyingine kule,aliongea mariamu
Aah hongera sana mwanangu una akili sana na unajua kuzitumia,aliongea baba yake kwa furaha
Asante sana baba ila bila wewe nisingeweza,aliongea mariamu
Haya,alijibu baba yake mariamu aliaga na kurudi nyumbani kwake,alipofika alimkuta mumewe na mke mdogo wamekaa sebuleni waangalia televisioni alikaa kwenye sofa akawasalimu habari zenu
Salama,alijibu bi mdogo
Yusuph kesho naomba wewe na mkeo mtafute pa kwenda mimi nasafiri na nyumba inapangishwa aliongea na kuweka kituo
Unasafiri unaenda wapi na inapangishwa na nani?,aliuluza yusuph kwa mshangao
Naenda marekani kusoma na inapangishwa na baba mwenyewe,alijibu mariamu akasimama na kuekekea chumbani kupanga vitu vyake
Yusuph,aliita asha
Naam mke wangu,aliitika yusuph
Tutaenda kukaa wapi sasa?,aliuliza asha
Mke wangu ata sielewi acha nimpigie simu baba mkwe iliita ilipopokelewa mazungumzo yalikuwa hivi
Haloo
Shikamoo baba,alisalimu yusuph
Marahaba haujambo?,aliuliza baba mkwe
Sijambo baba mbona unataka kupangisha nyumba yangu bila ruksa yangu,aliuliza yusuph
Nyumba yako! Nyumba yako ipi??,aliuluza baba mkwe kwa mshangao
Si hii ninayokaa na mke wangu,alijibu yusuph kwa kujiamini
Sikia mwanangu hiyo nyumba sikukupa wewe wala anna na ndio maana ata hati za nyumba zimeandikwa jina langu si majina yenu bali nilitaka mzalishe ili mjenge  nyumba yenu lakini ikashindikana na kwa kuwa imeshindikana kuanzia leo hiyo sio nyumba yenu tena,aliongea baba mkwe
Baba ungetupa muda kidogo tungejenga ya kwetu,aliongea yusuph
Unajua kwanini niliwapa duka moja na si mawili kama shemeji yako?,aliuliza baba mkwe
Kiukweli sijui baba,alijibu yusuph
Unahisi kwanini shemeji yako kila nilichowapa kina majina yao tofauti na nyie?,aliuliza baba mkwe
Hapana sijui,alijibu yusuph
Basi acha nikupe sababu kuu mbili ya kwanza anna kakurupuka kuolewa hivyo hajui maisha ya ndoa yakoje tofauti na shemeji yako na mkewe na pili wewe ulimuoa anna kwasababu ya mali na si mapenzi ya dhati,nadhani umenielewa,aliongea baba mkwe kiukweli hakuna alichoongea cha uongo vyote vya ukweli alijikuta akikata simu tu bila kuongea xhochote maana alijiuliza kajuaje lengo lake kuwa ni hilo.
Mariamu(anna) alipomaliza kupanga vitu vyake alimuita dereva wakatoa na kuviweka kwenye gari walibeba  kila kitu wakatoa nje vitu ya yusuph na mkewe,wakaambia watoke je walipotoka mlango ukafungwa eeeh kwaheri sikuwezi,aliongea asha
mke wangu usiseme hivyo mwenzio kaniacha nawe wataka  jamani,aliuliza yusuph kwa upole
Nahitaji kulishwa na sio kulisha,aliondoka zake na kumuacha yusuph kasimama na kiukweli chaguo lake ni asha sio anna alilia sana kwa kumkosa asha akaamua kurudi kwa wazazi wake.

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 28
Inaendeleaa.......
Anna alifika kwa baba yake vitu vikaingizwa chumbani kwake na vingine stoo kesho take asubuhi safari ya arusha ilianza muda wote yusuph alikuwa akimpigia simu lakini hakupokea alibaki anaiangalia tu kulingana na kuchukizwa na matendo ya mumewe huyo aliuekuwa anampenda kuliko mwanaume yoyote duniani na alimuamini kwa kila kitu,alipofika arusha alibadili namba ya simu hivyo akawa hana wazo na yusuph wala mwanaume yoyote alichowaza ni pesa tu
Baba na mama wawilu walienda siku moja kumtembelea baba yao walipofika walimkuta analia sana tena amekaa chini baba kuna nini?,aliuliza mama wawili
Wazazi wako judith,aliongea huku akilia zaidi
Wazazi wangu! wamefanyaje baba mbona sikuelewi,aliongea judith huku nae akihisi kuchanganyikiwa na machozi yakimtoka
Mzee raphael hakujibu zaidi alimpa simu ambapo aliangalia akaona ajali ya gari ya wazazi wake ikiwa imegongwa na lori kwa haraka akachukua simu yake akawapigia wakawa hawapatikani akaanza kulia ata mumewe nae akawa analia hakuna aliyeweza kumbembeleza mwenzake kwa muda huo zaidi ya kulia tu.
Baba na mama kwanini mmeniacha peke yangu tena siku chache kabla ya kusherehekea kumbukumbu ya siku yangu ya kuzaliwa,mngesubiri japo hiyo siku ifike kuliko kuniacha wakati bado nawahitaji katika maisha yangu yote,nitakuwa mgenibwa nani mimi niliwazoea wazazi wangu na bila nyie mimi nisingekuwepo mbona mmeniacha mapema? Nitawaambia nini wajukuu zenu wakirudi likizo?,alilia sana mama wawili
Mke wangu naomba usikufuru kiukweli wazazi wetu tuliwapenda sana ila Mungu amewapenda zaidi na hakuna mtu atakayepinga kuhusu upendo tuliokuwa nao dhidi yao ila inatubidi wao watangulie na sisi tubakie,aliongea baba wawili
Niataongea na nani mimi nilijiona nimepata ndugu wa kushirikiana nao lakini leo mmeniacha mwenyewe inauma kiukweli na sikutegemea kama itakuwa mapema kiasi hiki,aliongea mzee raphael huku akilia kwa sauti kubwa mpaka majirani wakasikia wakaja.
Walipofik wakaambiwa kilichojili wakawanyamazisha japo ilikuwa ngumu kwqo kuelewa kilevwanachoambiwa upweke ulitawala mioyo naachozi yalitanda kwenue kope zao,mzee raphael jikaze wewe ndio baba wa familia inabidi uongoze msiba huu sasa itakuwaje kama unalia muda wote?,aliuliza mwenyekiti wa mtaa
Sawa mwenyekiti ila siwezi maana kila nikikumbuka jinsi nilivyoishi nao machozi yananitoka peke yake natamani kama wangerudi tena ila haiwezekani,aliongea mzre raphael huku akiendelea kulia japo kwasasa alilia kimyakimya machozi pekee yalionyesha analia
Pole sana mzee mwenzangu ila vumilia ili tujue tunafanyaje kuhusu msiba huu mzito,aliongea mzee mwingine
Sawa nimewaelewa,alijibu.mzee raphael nakufuta machozi yake
Japo hakutegemea kama ipo siku atakuwa mbali bali na wazazi hao wa mkwewe. Tararibu za msiba zilianza na cha kwanza kabisa mzee raphael,mwanae na watu wengine wanne walielekea hospitali ilipphifadhiwa miili ya ndugu zake hao,walipofika wakapelekwa chumba cha kuhifadhia miili na walipiangalia wakaona ni wenyewe japo waliumia vibaya lakini waliweza kuwatambua,walipigundua ni wenyewe wakaenda nyumbani ambapo maturubai yakawekwa na mikeka na chakula kikapikwa,kutokana na uchungu aliokuwa nao judith hakuweza kula kitu chochote kile kwa muda ule uchungu wa kupoteza wazazi wake ulimfanya asisikie njaa.
Anna aliyekuwa arusha usiku huo alikuwa akiangalia televisioni ambapo alipata taarifa ya ajali iliyoua wawili mtu na mkewe wakataja na majina yao alishtuka sana akapiga simu ya kaka yake haikupokelewa,akapiga ya baba yake haikupokelewa akaamua asubuhi ya siku inayofuata aende zake dar,usiku huo hakulala muda wote alimuwaza wifi yake tu masikini wifi yangu sijui atakuwa na hali gani uko aliko ama kweli duniani tunapita,aliongea anna huku machozi yakimtoka
Asubuhi saa 10:30 alfajiri anna aliamka akaenda stendi ya mkoa arusha akapanda basi la kuelekea dar es salaam,saa 11:30 jioni alikuwa dar es salaam akakodi gari ndogo ikamfikisha mpaka kwao.

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 29
Inaendeleaaa......
Alikuta watu wengi sana nyumbani kwao ambapo aliingia ndani akaweka mkoba wake akaanza kumtafuta wifi yake alipo wakati akiendelea kumtafuta ghafla alitokea wifi yake mbele anna wazazi wangu wameenda sitowaona tena mimi,nitawapata wapi wazazi wengine mimi ee Mungu mbona umewachukua mapema yote hii,aliongea mama wawili huku kamkumbatia wifi yake wote wakaanza kulia anna alimkumbuka mama yake alivyowaacha peke yao tena wakiwa wadogo sana alilia sana hasa ukizingatia upweke atakaokuwa nao wifi yako na pengine kubwa halilolipata wifi yake kipenzi
Siku iliyofuata taratibu za mazishi zilifanyika watu waliaga miili ya marehemu bila kuona sura zao maana majeneza yao yalifungwa,waliaga walipomaliza wakarudi nyumbani kwa mzee raphael kiukweli upweke mkubwa ulitawala ns muda wote huo mama wawili analia picha ya wazazi wake ilizidi.kumrudia kichwani mwake anna alimliwaza wifi yake na muda wote alikuwa karibu nae.
Maisha ya amani,furaha kwa mama wawili yalibadilika kabisa na ukumbuke muda huo wanae walikuwa hawafahamu chochote kuhusu msiba huo,baada ya miezi mitano kupita mapacha hawa walifunga shule wakarudi likizo na wakati huo anna alikuwa karudi arusha na babu yao mzee raphael walikuwa wanaendelea na biashara zao pamoja na baba yao alikuwa dukani kwake huku mama yao akiwa nyumbani,walifika wakagonga mlango ngongongo
Karibu aliitikia mama yao aliyekuwa sebuleni alinyanyuka akafungua mlango waoo wanangu karibuni sana jamani,aliongea mama yao akiwakumbatia
Waoo mama nao walisema wakamkumbatia mama yao kwa furaha kubwa kutokana na kutomuona muda mrefu
Karibuni ndani wanangu,alisema mama yao akawapokea mabegi akaingizwa vyumbani mwao wakaketi sebuleni na baada ya dakika tano mama yao akarudi sebuleni
Poleni na safari watoto wangu,aliongea mama yao baada ya kuketi
Asante mama tumeishapoa ila tupeleke kwa bibi na babu tukawasalimie,alisema jackline alionyesha kuchoka sana na safari sana
Mtaenda kuwaona ila subirini nitawapeleka kw babu yenu mzaa baba yenu atawapeleka  yeye huko,aliongea mama yao
Twende sasa hivi mama tumewakumbuka sana,alisema jackson
Tutaenda saa 10 jioni muda huu babu yenu yuko kazini,muda huo ilikuwa ni saa 6 mchana,aliongea mama yao
Sawa mama ngoja nikaoge nipumzike kidogo,alisema jackline
Sasa si ule kwanza,aliongea mama yake
Hapana mama,alijibu jackline akanyanyuka na kuelekea chumbani kwake akalala jackline ni mbovu sana wa usingizi hivyo alivyojilaza tu usingizi ulimpitia muda ule ule,jackson mwanangu vipi habari za shule?,aliuliza mama yake
Nzuri tu mama sijui za hapa?,alijibu jackson
Nzuri tu chakula tayari karibu mezani,aliongea mama yake
Sawa mama asante sana,alijibu akanyanyuka na mama yake akanyanyuka wakaelekea meza ya chakula wakaketi mama yake akampakulia chakula nae akapakua wakala walipomaliza akaosha vyombo akarudi sebuleni wakaketi na ilipofika saa 8:30 mchana mama yao alinyanyuka akaenda kumuamsha baada ya muda mfupi jackline aliamka akaoga alipomaliza akaenda sebuleni akaketi kwenye meza ya chakula  akapakua chakula akala alipomaliza akaosha chombo akaelekea sebuleni akakaa na mama yake na kaka yake,kaka yake alinyanyuka akaenda kuoga alipotoka akamwambia mama yake tupeleke sasa
Sawa subiri nijiandae aliingia chumbani kwake akaoga alipomaliza akatoka wakaondoka kuelekea kwa babu yao mzaa baba yao ilichukua lisaa limoja  na nusu usiku wakawa wamefika kwenye safari yao
Waligonga mlango ngongo
Karibu,aliitikia mfanyakazi wa ndani wa mzee raphael

No comments:

Post a Comment