STORY:BABA NTILIE MGANE 18,19,20

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 18
Inaendeleaaaa...............
Judith?,aliita james
Abee james,aliitika judith
Nakupenda mke wangu,aliongea james akimshika mkewe usoni
Asante mume wangu nakupenda zaidi na nakuthamini kuliko kitu chochote wewe ni wa thamani zaidi kwangu,alijibu judith
Asante mke wangu kipenzi aliongea james na kumbusu mkewe huyu aliendelea kucheza mpaka alipofika kwa bibi ambapo alikuta bibi yuko kama alivyomuacha hajachezewa na mtu mwingine alimbusu mke wake mabusu mfululizo huku akimwambia nakupenda,nakuheshimu na nakuthamini mke wangu kipenzi sitokuacha wala kukusaliti tena,nakuambia ukweli mke wangu naomba uniamini sina mwingine zaidi yako na wala sitatamani mwingine,aliongea james wakati huo judith hakuwa na hali tena alisubiri kunyolewa tu maana hakuweza kuendelea kusuka zile nywele kwakuwa hazikutakiwa tena kwa wakati huo,james alizidisha utundu kitu kilichofanya kuku wa judith kuanza kutoa machozi ndipo alipoamua kumnyoa mkewe huyo alimnyoa vizuri mpaka alipohakikisha manyoya yameisha akamuacha.asante mume wangu kwa kuninyoa vizuri nakupenda sana mpenzi,alisema judith huku akilia kwa kuamini wazi penzi hili tamu la mumewe walishirikiana na msichana yule aliyekuja kuchukua nguo zake chumbani kwa mpenzi wake huyu.
Usilie mke wangu inatakiwa ufurahi ni siku tuliyoingoja kwa hamu kubwa na leo imetimia,aliongea james akimfuta machozi mkewe
Sawa mume wangu aliitikia judith lakini kiukweli aliumia na kitendo cha mumewe kumsaliti wakati wakiwa kwenye uchumba.walilala furaha,amani na upendo na wote walifurahi fungate lao walipomaliza fungate walifuatwa asubuhi na gari mpaka nyumbani kwao walishushwa wakafungua geti la nyumba yao wakaingia wakafungua mlango wa ndani kwao nyumba ilikuwa nzuri sana walifurahi kufika pale na kuona maisha kwao yatakua mazuri na rahisi sana.
Karibu nyumbani mke wangu kipenzi,alisema james walikagua nyumba na kuingia chumbani kwao ambapo judith alijitupa kitandani kutokana na uchovu aliokuwa nao,walishinda ndani siku hiyo na kesho yake asubuhi waliamka judith alipika chai baada ya kumaliza akaandaa maji yakuoga mumewe alipomaliza alimfata akamwambia maji tayari.
Asante mke wangu aliinuka james akaenda kuoga alipomaliza akapaka mafuta na kuvaa pensi na tisheti nyepesi wakaelekea mezani wakanywa chai walipomaliza wakaanza kufungua zawadi zao zilikuwa nyingi mno zikiwemo kadi,pesa na zingine nyingi. Mzee raphael alipiga simu kwa james iliita kwa muda kama mara mbili hivi baadae ilipokelewa na mazungumzo yakawa hivi haloo baba
Haloo haujambo?,aliuliza mzee raphael
Sijambo shikamoo baba,alijibu james
Mwenzio hajambo?,aliuliza mzee raphael
Hajambo yuko hapa,alijibu james
Mpe simu niongee nae,aliagiza mzee raphael
Haloo baba shikamoo,alisalimia judith
Marahaba haujambo wewe?,alijibu mzee raphael
Sijambo baba,alijibu judith
Sawa nakuja kesho nitakuja kuwachukua ili niwapeleke kwenye maduka yenu,aliongea mzee raphael
Sawa baba,alijibu judith
Mwambie mumeo pia,aliagiza mzee raphael akakata simu
Mume wangu kesho baba atakuja kutuchukua kutupeleka kwenye maduka yetu,aliongea judith huku akimuangalia mumewe
Sawa mke wangu tutakwenda,alijibu james
Walilala kulipopambazuka mzee raphael alikuja akawachukua na kuwapeleka duka la nguo na vipodozi alimkabidhi judith na lile la vyombo na mahitaji ya nyumbani alimkabidhi james walifungua biashara siku hiyohiyo kutokana na hamu waliyokuwa nayo ya kufanya biashara.

STORI:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 19
Inaendeleaaaaaa.........
Maisha yalianza kuwa mazuri sana kwao walifurahia sana maisha yao,miezi mitatu baadae judith alianza kuumwa na kurudisha chenji kwa kila kitu anachokula ata yawe maji au tunda hali ilikuwa hivyohivyo aliteseka sana mumewe akaamua ampeleke hospitali ili akajue tatizo ni nini,uko alipimwa akatoka nje kusubiri majibu baada ya nusu saa daktari alimuita judith aliitika alinyanyuka na kuingia kwenye chumba cha daktari alipofika akakaribishwa kiti akaketi,hongera sana mama,aliongea daktari
Hongera ya nini?,aliuliza judith kwa mshangao
Aliyekuleta nani yako na anaitwa nani?,aliuliza daktari
Ni mume wangu anaitwa james,alijibu judith huku bado akiwa haelewi nini kinaendelea daktari alinyanyuka akafungua mlango akaita james
Naam james aliitika akanyanyuka na kuingia chumba cha daktari alipofika akakaribishwa kiti akaketi na daktari bila kuchelewa akawaambia hongereni sana mkeo ni mjamzito,aliongea daktari
What are you sure?(nini? Unamaanisha?), aliuliza james kwa mshangao uliojawa furaha ndani yake
Ndio mkeo ana ujauzito wa miezi miwili,alijibu daktari kwa kuonyesha jinsi gani ana uhakika na anachokisema
Mimi daktari?,aliuliza judith aliyekuwa ameduwaa muda wote kana kwamba alikuwa amelala usingizi
Ndio wewe,alijibu daktari
Asante Mungu lakini kwanini nashindwa kula?,aliuliza judith
Hiyo hali huwa inatokea nitakupa vidonge vya kupunguza kama si kumaliza kabisa hiyo hali,aliongea daktari akachukua peni na karatasi akawaandikia dawa wakaenda kupeleka karatasi mapokezi walipatiwa dawa wakalipia wakaondoka,njia nzima james hakuamini alihisi kama anawaza iwe hivyo alimuangalia mkewe na kumwambia nakupenda sana mke wangu tena zaidi ya ninavyojipenda mimi kipenzi changu,aliongea james akitabasamu
Asante mume wangu nakupenda zaidi ya unavyofikiria wa moyo wangu na hakuna kama wewe alijibu judith kwa furaha
Walifurahi sana mimba ilipofikisha miezi minne judith alianza kula kama kawaida tena bila mpangilio wala kufuata ratiba mpaka mumewe akaanza kumshangaa,siku zilizidi kwenda mimba ilipofikisha miezi saba ndipo judith akaamua kumwambia mama yake juu ya hali yake alifurahi sana,kiukweli alikuwa makini sana na mimba yake na alifata ushauri wote wa daktari na mazoezi alifanya kama kawaida bila kujali mumewe yupo au hayupo,miezi tisa kasoro mama judith alikuja kukaa kwa mkwewe kwa ajili ya kumuangalia mwanae mpaka atakapojifungua awe nae karibu,siku ya siku iliyosubiriwa na familia ilifika judith alipata uchungu akapelekwa hospitali ambapo alijifungua watoto wawili mmoja wa kike na mwingine wakiume,babu zao,bibi yao na baba yao walifurahia sana ujio wa hawa watoto lakini katika hawa wote hakuna aliyekuwa amefurahi kumzidi anna ambaye alikuwa akipenda kubeba watoto hivyo alikuwa anabeba watoto wa watu na wengine wanamkatalia lakini hakujali alikuwa anawabeba ata kwa kuwaiba kwasasa aliona kilio chake kimejibiwa atakuwa anabeba watoto wa kaka yake ambao nae pia ni mama yao japo si mzazi,waliruhusiwa wakarudi nyumbani kule dukani kwa judith aliwekwa mfanyakazi na nyumbani akawekewa mfanyakazi muda mwingi judith alikuwa akicheza na watoto wake na kuwafanya muda wote wawe na furaha. Hatimaye watoto hawa mapacha walifikisha miaka mitatu baba yao aliwafungulia akaunti kila mtoto alimuwekea milioni tano kwa kila na pia mama yao alifungua saluni iliyokuwa inahudumia wanaume na wanawake iliandikwa jackline and jackson saluni,majina waliyopewa na babu yao mzee raphael aliwapenda sana wajukuu zake hawa,maisha yalikuwa ya furaha sana hatimaye walifikisha miaka minne mzee raphael aliwapeleka shule ya bweni wakati huo anna alikuwa amemaliza chuo na kuajiriwa nchini uganda japo baba yake alimkataza lakini hakusikiliza alikuwa mbishi na jeuri kupita kiasi na kuona baba yake anapenda kumuona amekaa tu hapo alipo kumbe mawazo na hisia zake vilimdanganya mzee raphael alitaka kumsaidia mwanae ili ajiajiri na kujitegemea mwenyewe.
Anna alikuwa hataki kusikia wala kuambiwa habari hizo za kujiajiri kwasababu yeye aliamini katika kuajiriwa zaidi kuliko kujiajiri,james alijaribu kuongea nae lakini hakumsikiliza pia zaidi ya kumwambia amuache kama alivyo maana yeye ana maisha yake na familia yake amuache nae atafute

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 20
Inaendeleaaaa................
James hakuwa na namna isipokuwa ni kumuacha mdogo wake aende uganda aliondoka na alipofika huko alianza maisha yake nchini humo huku akiapa kamwe hatoweza kumsumbua baba yake kuomba msaada wowote,wifi yake alijaribu kumwambia ata kama kitu hautaki usikatae kama unagombana na mtu sawa wifi yangu maisha hayaendi hivyo huenda siku ukakihitaji hicho kitu alafu mtu akakunyima utanilaumu?
Tatizo wananilazimisha nifanye wanayotaka ata kama sitaki nifanyeje sasa mimi?,alijibu anna kwa dharau na kuona kama wamemuonea
Usitumie ukali wifi yangu nakuomba tafadhali unajua yule ni mzazi wako na james ni kaka yako unadhani unavyowajibu jeuri wanajisikiaje?,aliongea mama wawili
Sijui na sitaki kujua kwani wao wanajua najisikiaje wanapolazimisha nifanye kitu nisichokitaka?,alijibu kwa jeuri na hasira
Sawa alijibu mama wawili kwa unyonge maana hakutegemea kama anna amebadilika kiasi hicho na kujibu jeuri kila mtu bila kujali ni baba mzazi mkubwa au ndugu na aliumia zaidi hasa ukizingatia baba yao aliwalea toka mama yao alipofariki na kuwasomesha mpaka hapo walipofika bila msaada wa mtu yoyote.
Mzee raphael aliumia kwa majibu mabaya ya mtoto wake ila alimsamehe maana alijua wazi hajui anachokifanya na ata akija kujua muda utakuwa umeishakwenda tayari,mwaka mmoja baada ya judith kuajiriwa uganda alipata ajali mbaya ya gari wenzie wote walifariki papo hapo yeye peke yake alipona simu ilipigwa kwa baba yake alifika uganda akampeleka india ambapo alitibiwa na kurudi kwenye hali yake ya kawaida akarudishwa moja kwa moja nchini Tanzania njia nzima alikuwa akilia mpaka wanafika kwao alikuwa hana amani kabisa huku akihisi baba yake anaweza akamfukuza lakini haikuwa hivyo baba yao aliwapenda sana watoto wake,walipofika waliketi kwenye sofa muda huohuo anna alipiga magoti na kumuomba msamaha baba yake nae bila hiyana wala kinyongo alimsamehe,wifi yake na kaka yake nao walikuja kwa ajili ya kumpa pole aliitikia akapiga magoti tena na kumwambia wifi yake nisamehe wifi yangu sitorudia tena najua kama ningewasikiliza yasingenikuta haya yote nisamehe sana kaka sitorudia tena,aliongea huku akilia
Walimuinua sisi tumekusamehe ila usirudie tena kaa ukijua mkubwa akikukatalia kitu ujue kina madhara kwako hivyo usiwe mkaidi,aliongea kaka yake
Sawa nimekuelewa siwezi fanya ukaidi tena nimeishajifunza,aliongea anna huku akilia wifi yake alichukua kitambaa chake akamfuta machozi na kumwambia asilie wamemsamehe kwani yeye ni mtoto wao na atabaki kuwa mtoto wao.
Miaka ilizidi kwenda huku jackline na jackson walizidi kusoma kwa bidii walikuwa darasa la tatu pesa kwao zilikuwa kama karatasi kutokana na pesa walizokuwa wameziandaa wazazi wao kwa ajili yao na babu yao pia,kiukweli walikuwa wadogo lakini walikuwa na matumizi makubwa ya hela yasio na msingi kiasi kwamba watu wengi waliamini baba yao atakuwa ni mtu mkubwa serikalini kumbe la hasha ni kujiwekea malengo na akiba mara tu watoto wanapozaliwa kabla ata hawajaanza kusoma tofauti na wazazi wengi ambao usubiri mtoto aanze shule ndio waanze kuangaika kutafuta ada ya kusomesha mtoto na hapo wengi ndio ufeli kutokana na kukosa maandalizi ya mapema.
Walipofika darasa la tano walimu waliamua kumuita mzazi wao ambapo mama wawili alifika shuleni akaenda moja kwa moja ofisi ya mkuu wa shule alipofika akakaribishwa kwenye kiti akaketi
Asante mkuu wa shule mimi ni mzazi wa jackline na jackson james nimepokea barua ya kuitwa ndio nimekuja kuitikia wito,alisema mama jackline
Asante kwa kuitikia wito kikubwa tumekuita hapa ili tukuambie tumechoshwa na matumizi mabaya ya pesa ya watoto wako maana wanawakosesha raha wenzao,alisema mkuu wa shule.
Itaendeleaaaa

No comments:

Post a Comment