STORY:BABA NTILIE MGANE 21,22,23 na 24

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 21
Inaendeleaaaaaa........
Matumizi makubwa yapi na kwenye nini?,aliuliza mama wawili
Wananunua vitu vya gharama ambavyo wenzao hawawezi kumiliki hauoni kama wanawakosesha amani wenzao ambao hawana uwezo wa kumiliki vitu hivyo?,aliuliza mkuu wa shule
Samahani mwalimu kwani wanasoma au hawasomi?,aliuliza mama wawili bila kujibu swali la mkuu wa shule
Wanasoma ila tatizo matumizi yao kipesa ndio mabaya,aliongea mkuu wa shule kwa kujiamini
Kwahiyo tufanyeje?,aliuliza mama wawili maana alimuona mwalimu mkuu hana akili timamu kumuita kote kwa barua kumbe na kumpigia simu kumsisitiza asikose anamuitia ujinga
Wapunguzie kiwango cha pesa unachowapa na kama haiwezekani wahamishe shule tu,aliongea mkuu wa shule kwa kujiamini
Sawa waandikie uhamisho,aliongea mama wawili kwa ujasiri mkubwa
Haya sawa wanahamia wapi?,aliuliza mkuu wa shule kwa mshawasha wa kutaka kujua
Wanahamia Afrika kusini kwenye shule ile ya wazungu na watu wanaojiweza tu kwasababu siwezi punguza matumizi sitoi mimi anaetoa ni babu yao,aliongea mama wawili kwa kujiamini
Mmh babu yao!!! Babu yao anaitwa nani?,aliuliza mkuu wa shule kwa mshangao
Anaitwa Raphael Jonathan,alijibu mama wawili
Raphael jonathan yupi huyu mfanyabiashara mkubwa au?,aliuliza mkuu wa shule
Ndio huyo huyo,alijibu mama wawili
Sawa basi wala usiwahamishe ni haki yao ata hivyo wanaibeba sana shule kwenye mitihani ya shule na ata ya kushindana na shule zingine,aliongea mkuu wa shule.kwa upole sana
Sawa kwaheri,aliongea mama wawili akanyanyuka na kuondoka,alipofika nyumbani alimkuta wifi yake akamsalimia na kuketi sofani
Pole wifi maana umechoka hatari,aliongea anna
Yaani we acha tu wifi yangu nilidhani wananiitia kitu cha maana eti wananiambia tupunguze bajeti ya hela tunazowapa watoto,aliongea mama wawili
Eeh kukusumbua kote uko?,aliuluza anna kwa mshangao
Ndio tena wakaniambia nikishindwa niwahamishe kabisa maana wanawatesa wenzao ambao hawana pesa au ni masikini,alielezea mama wawili
Ukawaambiaje sasa?,aliuliza anna akikaa mkao wa kusikiliza vizuri jibu la wifiye
Nilikubali na kuwaambia nitawahamisha maana uwezo wa kupunguza pesa za matumizi sina kwasababu si mimi ninaewapa,aliongea mama wawili
Umefanya vizuri kwahiyo wameandika uhamisho?,aliuliza anna
Waliniuliza nani anawapa nikawaambia wakasema eti oooh msiwahamishe huwa wanaibeba shule,walikuwa wanatikisa kibiriti kama kinanjiti wamekuta zimejaa,aliongea mama wawili
Eeeh hawa walimu wengine bwana sijui wanasomea wapi??,aliuliza anna
Hapo mimi na wewe hatujui,alijibu mama wawili na kuongeza umepika nini maana hadi njaa inaniuma,aliuliza mama wawili
Nimepika ugali,dagaa na mchicha,alijibu anna
Waouh afadhali umejuaje napenda sana hizo mboga,aliongea mama wawili kwa furaha akainuka na kuelekea meza ya chakula alifunua hotpot la kuhifadhia chakula akakata ugali akafunika akafunua ya mboga akapakua akayafunika,akaketi kwenye kiti alipomaliza akaelekea jikoni akasuuza sahani na kuirudisha kwenye kabati la jikoni,akaingia chumbani kwake akajimwagia maji alipomaliza akabadili nguo akarudi sebuleni akaketi wakaanza kuangalia filamu,waliangalia mpaka mumewe akarudi alimpokea akamuwekea maji ya kuoga alipooga akapumzika chumbani kwao maana bafu na choo vilikuwa humohumo mkewe nae akaketi kitandani pole na kazi mume wangu
Asante sana mke wangu imekuaje shuleni?,aliuliza mumewe
Hamna kubwa sana ni la kawaida tu akamuelezea ilivyokuwa mumewe alicheka sana ,akamuomba mkewe apumzike kidogo kweli mama wawili alitoka akaenda jikoni kuandaa chakula cha usiku.

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 22
Inaendeleaaa........
Walipika walipomaliza alienda chumbani kwao wakati huo anna alikuwa anaandaa mezani,alimuamsha mumewe wakala na kuelekea kulala anna nae akaenda kulala,anna aliyapenda sana maisha ya kaka yake na wifi yake mara nyingi alipokuwa akiwaona alitamani nae aoleww na mwanaume atakaemjali,kumthamini na kumheshimu kama ilivyo kwa kaka yake lakini swali lake lilikuwa je atampata wapi?,alizidi kuumia kila siku na akitamani sana kuolewa mpaka wakati huo hakuwa na mwanaume yoyote yule na alipanga amdanganye wifi yake,akaamua kumueleza wifi yake uongo huo natamani sana kuolewa tena zaidi ya sana na mwanaume atakaeniona natamani awe kama kaka ila kiukweli mpaka sasa sijaona atakaefanana nae,kingine naogopa sana maana sijawahi tembea na mwanaume yoyote,aliongea anna akitegemea wifi yake atakubali uongo huo
Mmh wifi yangu unajua shida si kuolewa tatizo ni je mwanaume atakaekuoa atakujali na kukuthamini wakati wote bila kujali kwenu mko vipi wala wewe uko vipi?,aliongea wifi
Kwetu kivipi wifi?,aliuliza anna
Unajua baba ni tajiri sana na kwasasa kupata mwanaume atakayekupenda kwa dhati na si kupenda mali zenu ni ngumu mno au kuna mwanaume yoyote ambaye hajui kwenu mko vipi na anaonyesha upendo wa dhati?,aliongea wifi mtu na kuuliza
Kuna mkaka mmoja anaitwa japhet nimesoma nae chuo alionyesha kunipenda ila sikuwa na mpango nae maana niliogopa kuchezewa,alijibu anna kwa kujiamini
Aaaah una uhakika haumjui mwanaume?,aliuliza wifi yake kwa mshangao mkubwa
Ndio wifi kwanini nikudanganye?,aliongea anna na kuuliza swali
Sawa najua huenda umesahau au unajisaulisha wewe haukutoa mimba wakati ulipokuwa shule je,iliingiaje ikiwa haumjui mwanaume na pia yusuph huyu wa nyumba ya pili haujawahi tembea nae tena si mara moja?,aliuljza wifi mtu maswali mfululizo
Mmh wifi hayo yashapita ila nataka kuolewa sasa hivi ili nitulie,alijibalaguza baada ya kuona uongo wake haujazaa matunda
Oooh kwahiyo usipoolewa na hautotulia au sijaelewa? na je nani kakwambia utulivu unapatikana kwebye ndoa?,aliuliza wifi yake
Mmmh sijui ila naamini nikiolewa nitatulia,alijibu anna
Sawa ila ushauri wa bure ukiupenda uchukue usipoupenda uache acha kwenda kumbi za starehe,acha nguo za nusu utupu,acha kujiona wa ulaya pia kuishi maisha ya ulaya,achq kuringa atakaekuzika au kubeba jeneza lako haumjui na kujiona wewe mzuri hakuna kama wewe na acha kutukana watu hovyo na kutumia mwili wako hovyo,aliongea wifi yake
Kuutumia mwili wangu vibaya vipi? Na nimetumiaje vibaya?,aliongea kwa hasira anna maana ili lilimuuma kuliko yote
Wala usikasirike wifi yangu mimi ni kama rafiki yako ndio maana nakwambia na nakwambia kwasababu nakupenda la sivyo ningekuacha,ebu nielewe ukienda klabu jumapili unarudi jumatatu au jumanne je kuna vyumba vya kulala uko kama sio unakuwa umeolewa kwa muda?,aliongea wifi yake
Kiukweli hawa naenda kwa bwanangu na si mmoja nitakaekutana nae klabu naenda kulala nae kikubwa awe na pesa tu,aliongea anna lakini akionyesha hasira za wazi
Ili kuwa mke bora na si bora mke inatakiwa kwanza uuheshimu mwilu wako sana na uuthamini pia usiufanye kama choo cha stendi kwamba kila mwenye haja ataingia kujisaidia bila kujali awe mgonjwa au mzima ataingia tu,badilisha mavazi yako kutoka kuvaa nguo fupi kupindukia ambazo ata mtu akikuona anashindwa kukuelewa kwamba umevaa nguo au nguo ya ndani? na kuvaa nguo za heshima ambazo hazionyeshi maungo yako,aliongea wifi yake aliyekuwa akimshauri utafikiri mwanae wa kumzaa
Nikishabadilika itakuaje?,aliuliza anna swali la kitoto
Utapata mume bora pia si bora mume,alijibu wifi yake
Nianze lini kubadilika?,aliuliza anna
Mabadiliko ni wewe ukitaka hata sasa,kubadilika unaweza na ukishabadilika kaongee na baba unachotaka ufanye ili akufungulie kuliko kuomba pesa tu,aliongea wifi yake
Sawa wifi yangu nimekuelewa,aliongea anna kwa utii mkubwa
Itaendelea

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 23
Inaendeleaaaa....
Kesho yake asubuhi anna alienda madukani akanunua nguo ndefu zikiwemo sketi na blauzi na magauni,akapitia sehemu wanaposajilia line akasajili line mpya na kuvunja ile aliyokuwa nayo,alipomaliza akaenda kwa wifi yake hakumkuta alikuwa ametoka alikaa akaona amechoka akaenda chumbani kwake akaoga kuondoa uchovu akabadili nguo na kuvaa gauni lefu mpaka chini jekundu la kumwaga na kiatu kirefu cheusi alijiangalia kwenye kioo akaona bado hajapendeza akapaka vipodozi usoni na kubeba pochi yake nyekundu bila kusahau sikio lake akalipamba kwa heleni nyeusi alijithaminisha akajiona kweli kapendeza akatoka na kwenda nyumbani kwa baba yake kila alipopita walimshangaa wengine walijiuliza kapatwa na nini,alipofika nyumbani akagonga mlango mlinzi wao machachali mwenye utani mwingi akafungua mlango akamkaribisha karibu sana malkia nikusaidie nini?
Eeh wewe baba nimemkuta?,aliuliza anna
Mlinzi akabaki mdomo wazi alimuangalia kutoka juu mpaka chini eeh kumbe ni wewe dada Anna umependeza hadi nimekusahau mwenzako yaani moyo umeenda mbinguni kusalimia mara moja baada ya kukuona tu,aliongea mlinzi
Wewe baba yupo au hayupo?,aliuliza anna
Baa----ba yupo ama kweli watu mnabadilika umekuwa malkia yaani,anna akaenda akagonga mlango
Ingia uko wazi,alijibu baba yake aliyekuwa ameketi sebuleni
Anna aliingia akapiga magoti na kumuomba msamaha baba yake naomba baba unisamehe sana najua nimekukwaza mara nyingi nakuahidi sitorudia tena,aliongea anna
Anna ni wewe mama yangu ama kweli kwa wifi yako ni chuo cha mafunzo yaani mpaka umebadili mavazi,aliongea baba yake
Naomba baba unisamehe sana najua umeteseka sana kutusomesha na kutulea mpaka tukafikia hivi leo nisamehe sana,aliongea anna huku machozi yakimtoka
Baba yake alinyanyuka akamfuata binti yake akamuinya na kumkumbatia kwa nguvu huku nae machozi yakimtoka nimekusamehe mwanangu ata kama ukifanya kosa gani utabaki kuwa mwanangu,alisema baba yake
Asa.....nte sana baba,aliongea anna kwa sauti ya kwikwi nakuahidi kamwe sitokukera wala kukukwaza tena katika maisha yako yote,aliendelea kuongea anna
Nafurahi kama umelijua kosa lako,aliongea baba yake
Asante baba,aliongea anna waliachiana na baba yake akamwambia karibu sana mwanangu jisikie huru nimekusamehe na sina kinyingo nawe tena.
Asante sana baba,waliketi wakaongea mengi sana huku wakicheka na kufurahi,baba yake alifurahi sana kuona mwanae kavaa vazi la heshima tofauti na siku zote ambazo alikuwa anatamani ata afumbe macho kutokana na vivazi vifupi vya bintiye.katika siku zote leo umenifurahisha sana mwanangu?,aliongea baba yake
Kwanini baba?,aliuliza anna
Vazi lako tu ndio limenifurahisha,alijibu baba yake
Asante sana baba na nakuahidi utafurahi zaidi na zaidi,aliongea anna
Waliongea mengi sana huku baba yake akionyesha tabasamu muda wote baada ya masaa matatu kupita anna aliaga na kuondoka baba yake akamruhusu,alitoka akafunguliwa mlango na mlinzi akaondoka zake
Alipofika nyumbani  alimkuta wifi yake karudi alifungua mlango akaingia eeh wifi ni wewe?,aliuliza wifi yake
Ndio wifi,alijibu anna
Umependeza hadi raha yaani,aliongea wifi yake
Asante,shikamoo,alisalimu anna
Marahaba haujambo wewe?,aliitikia wifi
Sijambo unasalimiwa na baba,nimeishamuomba msamaha kanisamehe,alijibu anna
Eeh kasemaje alivyokuona?,aliuliza wifi yake
Kanishangaa pia na kuniambia nimependeza sana,aliongea

STORY:BABA NTILIE MGANE
MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 24
Inaendeleaaa......
Mabadiliko ya ghafla ya anna yaliwashangaza watu wengi na ata marafiki.zake walipokuja ili watoke nae kwenda sehemu za starehe aliwakatalia katakata,baadhi wakahisi kalogwa kwakuwa ata nguo zake.za ajabu aligawa kwa watu bila kujali bei ya hizo nguo alichokijali hazihitaji tena na hazina maana kwake.
Miezi sita baadae barua za kumposa anna zilianza kugonga hodi kwenye nyumba ya mzee raphael na wachumba wakishindana kila mtu akitaka aonekane yuko.zaidi ya mwenzie,wapo waliokuja na mapikipiki,wapo waliokuja na magari,wapo waliokuja kwa baiskeli na wengine walikuja kwa miguu,anna hakumpenda ata mmoja wao isipokuwa yusuph ambae alikuja kwa miguu alikubali ombi la yusuph na akabadili dini akaitwa mariamu wakafunga ndoa ya kiislamu,walipewa zawadi.ya nyumba na duka la viatu walifurahi sana huku mariamu(anna) akifurahi na kuamini ushauri wa wifi yake umefanya kazi.
Mariamu(anna) alianza maisha ya ndoa na yusuph huku akiamini ndiye mwanaume pekee anaeweza kupanga nae maisha bila kujua yusuph alitamani mali tu na si yeye na kiukweli hakumpenda anna ata kidogo ila alimpenda sana asha binti wa kipare ambaye walikuwa wapenzi muda mrefu na asha alijua.kuhusu ndoa ile ila kwakuwa wanahitaji kupata mali hakuongea kitu chochote wala kupinga ndoa hiyo,yusuph mudq mwingi alikuwa bize na simu yake bila mkewe kujua anawasiliana.na nani? Ata mapenzi aliyokuwa akionyesha kwa mkewe yalipungua huku akiamini hati ya nyumba imeandikwa majina yao wote wawili hivyo ni rahisi sana kwake kumuacha yule binti na wakagawana nusu kwa nusu mke wangu aliita yusuph
Abee mume wangu,aliitika mariamu(anna) kwa unyenyekevu mkubwa
Nahitaji kuongeza mke wa pili,alijibu yusuph
Unahitaji kufanya nini?,aliuliza mariamu kwa mshangao
Nahitaji kuoa mke wa pili,alijibu yusuph kwa kujiamini
Kwasababu zipi?,aliuliza mariamu
Dini inaruhusu na pia nahitaji upate mtu wa kukusaidia majukumu,aliongea yusuph
Unakumbuka uliniambia nitakuwa peke yangu wala hautatamani mwingine leo imekuwaje utake kuoa mke wa pili,aliongea mariamu
Hayo yalikuwa maneno tu ila ukweli nataka kuongeza mke wa pili na kama hautaki tuachane tu,aliongea yusuph kwa jeuri
Unatafuta sababu ya kuachana nami si ndio?,aliuliza mariamu baada ya kauli ya mumewe kumshangaza
Sio natafuta sababu ukikubali muwe wawili sikuachi ila bila hivyo nakuacha,aliongea yusuph kwa msisitizo
Sawa nitakujibu kesho,alijibu mariamu na kulala
Haya aliongea yusuph akaendelea kuchati na asha toka amemuoa mariamu hajawahi mpa haki ya ndoa kiasi kwamba mariamu alijuta kwanini aliolewa.
Kulipokucha aliamka akaoga akajipara na kupendeza alipomaliza akaenda moja kwa moja dukani kwa wifi yake,macho yake yalikuwa mekundu na yameiva kutokana na kulia usiku mzima,alipofika akamsalimu wifi yake shikamoo wifi
Marahaba mbona hivyo kwema utokako?,aliitikia salamu na kuuliza swali
Sio kwema kabisa wifi yangu yaani yusuph anataka kuoa mke mwingine,aliongea mariamu huku akilia
Eeh pole sana wifi njoo ndani tuongee alimshika mkono wakaingia kwenye chumba ambacho huwa anabadilishia nguo,wakaketi haya niambie umejuaje au umesikia?
Bora ningesikia kaniambia mwenyewe kwa kinywa chake,alijibu mariamu
Umemkosea au?,aliuliza wifi mtu
Sijawahi ata mara moja navumilia mengi sana kwake kiasi kwamba mpaka muda mwingine naona nilikurupuka kuoana nae,usiku mzima anachati hana muda na mimi kabisa lakini nimevumilia mbaya zaidi toka kanioa hajawahi nipa haki yangu ya ndoa napo nimevumilia alafu leo eti anataka kuo...... alishindwa kumalizia akaishia kulia
Nyamaza wifi yangu pole sana najua unaumia sana lakini hayo yote ni mapito tu na mitihani ya ndoa yatapita tu,aliongea wifi yake
Sawa lakini sidhani wifi nateseka mimi aliongea mariamu kwa uchungu

No comments:

Post a Comment