STORY:NILITUMIWA NA WACHAWI BILA KUJUA MTUNZI:ESTER MWAKABONGA SEHEMU YA 18 Inaendeleaaaaa...................

Alifika mama happy akagonga mlango ngongongo
Karibu,aliitikia baba huku akiuendea mlango,alifungua aaah kumbe wewe karibu shemeji
Asante sana alijibu mama happy huku akiingia ndani,huyu mwanamke nilikuwa namtamani kila siku,kweli ndege mjanja unasa kwenye tundu bovu,aliongea baba huku akifunga mlango
Waliingia chumbani wakakaa kitandani,baba akamwambia mama happy tuingie uanjane jiandae,mama happy akasaula na baba akasaula wakabaki kama walivyotoka kwenye matumbo ya mama zao walipomaliza wakapanda kitandani ili waanze kucheza mechi na wapate mshindi wa mechi hiyo,kabla hawajaanza kufanya chochote makofi yakapigwa paapaa paapaa wote wakashtuka nini hiki walipoangaza ndipo wakawaona watu wanne wamekaa kila mmoja kwenye pembe yake,mamaa,nyie akina huku akitetemeka na kujimwagia maji kwenye suruali yake,mama alikuwa anatetemeka tu,mbona hamjibu?,aliuliza baba
Endeleeni nyie si majasiri,waliongea wale watu
Mama alitetemeka mno mpaka wakahisi anahoma,we mwanamke vaa haraka ukimbie,mama happy alikubali akavaa haraka akakimbia.
Baba alikaa kimya hakuthubutu kufungua kinywa chake,haya ndiyo maisha uliyoyachagua? na  unajua mĂ dhara yake,aliulizwa baba lakini hakujibu alikaa kimya,nenda kaoge haraka uingie kwenye chumba alichokuwa anatibiwa mkeo
Sawa baba alijibu,kisha akaenda kuoga alipomaliza akaingia kwenye kile chumba,lala chini watu walimwamuru baba nae akupinga akalala,aliota yuko sehemu nzur,kuna nyumba nzuri,badae akaonyesha anazika tena akiwa hai,akashtuka nisameheni sitorudia tena,aliongea baba huku akilia kwa uchungu.
Wakamrudisha kwenye fahamu zake,ukirudia mimba aliyobeba mkeo utabeba wewe,waliongea wale watu kisha wakapotea.Baba alikimbia mpaka nje akaanza kuogopa kuingia ndani.
Mama happy alifika kwake huku akijiuliza wale ni wakina nani?,ghafla wakatokea ukutani akawatazama usoni mwao ili macho yalikuwa yanang'aa kama jua la kiangazi,alishindwa kuvumilia akaanguka,akawa anaota yuko kwenye msitu mkubwa hajawahi uona,una wanyama wakali,mafuvu,mifupa na vitu vingine,akaanza kutembea alipotoa mguu alitokea mtu ameoza mwili mzma na funza wanadondoka,akaongeza mwendo ukatoka mguu,akaanza kukimbia huku nyuma wakawa wanamkimbiza wale wenye funza na viungo,unaenda wakati,akaulizwa mama happy,hakujibu akawa anakimbia tu,mbele akaona simba,chui,kushoto akaona chatu wengi na kulia akaona watu warefu sana nguvu zikamwishia wale wote wakamzunguka akalia mamaaaa,akashtuka akajikuta alichokiota kimetokea,nisameheni mnirudishe kwa mtoto wangu aliongea mama happy kwa uchungu
Hapa ndipo utakapoishi kuanzia leo,uliongea mguu
Nisamehe naombeni,alibembeleza mama happy
Hahaha,walicheka kisha wakarudi sakafuni.
Itaendelea.......
KWA MAONI NA USHAURI
NO:0712634865
       0752064667
EMAIL:estermwakabonga@gmail.com

No comments:

Post a Comment