STORY:BABA NTILIE MGANE

MTUNZI:ESTER H.MWAKABONGA
SEHEMU YA 15
Inaendeleaaaa..........
Nisamehe james sitorudia tena nakuahidi,alisema sarahia huku akilia maana kadri muda ulivyokwenda ndivyo james alivyozidisha kipigo mpaka akamuumiza.
Mamaaaa unaniumiza james,aliongea sarahia kwa sauti kubwa mpaka wakashtuka wakaja walimzuia james lakini hakusikia sarahia alipoona hivyo akajidondosha ili wajue amezimia.James akaondoka zake akaelekea bwenini huku akilia kwa sauti  mpaka wanachuo wenzie wakawa wanamshangaa kuwa imekuwaje,jonathan alimuona james kuwa hayuko sawa akamfuata na kumuuliza imekuwaje james?
Kamuulize demu wako,alijibu james huku akiendelea kutembea kuelekea chumbani kwake alipofika alijitupa kitandani huku akizidi kuongeza sauti maana alijua wazi mwanamke wa maisha yake amemkosa kwa tamaa zake za kimwili na hakutaka kuamini kilichotokea.
Jonathan alisimama baadae akaamua kwenda chumbani kwa sarahia alipofika alimkuta sarahia yuko chini huku wenzake wakimpepea alimuita lakini wapi baada ya dakika kama 15 au 20 sarahia alizinduka na kuhisi maumivu makali sana mkononi,alipogeuka alimuona jonathan alimkumbatia huku akilia kwa hasira,nisamehe jonathan kwa yote niliyoyafanya sikutegemea kama nitaharibu mahusiano ya james na mchumba wake kipenzi aliyempenda kuliko ata mimi,naomba kaniombee msamaha ataniua mimi yule maana bila mimi kuanguka asingeniacha,aliongea sarahia
Pole sana kwani umemfanya nini wewe nawe?,aliuliza jonathan kwa sauti ya upole
Jana nilienda kuchukua nguo zangu na picha nikamkuta james na mwanamke mimi nikapitiliza kwenda kuchukua bila ata kupiga hodi ndipo mkewe akaamua kuondoka,james kaja leo kunipiga kwa ajili ya hilo,aliongea sarahia
Sawa nitaongea nae,alisema jonathan akamketisha sarahia kitandani akaondoka zake,visa na ugomvi kati ya sarahia,jonathan na james uliendelea huku james akihisi jonathan alimtuma sarahia kufanya vile kutokana na utetezi wake juu ya binti huyo,sarahia akupenda ugomvi ata kidogo aliamua kuhama chuo na kuondoka kabisa nchi hiyo akaenda kusoma afrika kusini.
Judith alifika uwanja wa ndege akachukua teksi mpaka chuoni kwao alipofika karibu marafiki zake wote walimuuliza kulikoni mbona hivyo hakujibu alikaa kimya tu na kuwapita kama hawajui macho yake yalikuwa mekundu ule weupe wote uliisha na yalivimba sana kutokana na kulia njia nzima,aliapa kumuumiza james pia alikaa akalia sana hivi huyu mwanaume mbona amenifanyia hivi nimemkosea nini mimi?,alijiuliza judith lazima kuna kitu nimemkosea huenda kwa bahati mbaya lakini ata kama ndio anifanyie hivi jamani kosa langu nini mimi? Dah ngoja nami nimsaliti ili nijue utamu wake maana huenda kuna faida.
Maisha yalibadilika kwako alianza kuishi maisha yakumtega mkuu wa chuo kiasi kwamba mkuu wa chuo akakubali na kuamua kupanga siku ya kulila tunda la binti huyu mrembo kutoka Tanzania. Ilikuwa siku ya jumamosi judith alivaa vizuri na akapendeza hadi wasichana wenzie wakaanza kumuonea wivu na wengine kumsifia umependeza judaith
Asanteni jamani,alijibu huku akiendelea kutembea kuelekea nje ya geti hapo alichukua teksi akapelekwa mpaka hotelini ambapo mkuu wa chuo alikuwa tayari ameishafika,alipofika alilipa hela ya teksi akaingia mapokezi akaenda kulia akaona lifti akapanda mpaka ghorofa ya 7 chumba namba 12 akagonga mlango,mkuu wa chuo akafungua mtoto mzuri akazama ndani akaufunga mlango.
Mmmh umependeza jamani hadi raha mpenzi wangu mmwaaaah,aliongea mkuu wa chuo na kumbusu shavuni
Asante mpe.....,alishindwa kumalizia akajikuta akilia tuu
Nini tena mpenzi?,aliuliza mkuu huyu ambae furaha yake yote iliyeyuka ghafla baada ya kusikia kilio cha mrembo huyu na kuona chozi likimwagika
Hamna kitu,alijibu judith huku akijilazimisha kucheka lakini haikuwa rahisi maana macho yake yalikataa
Mmmh nambie mama,alizidi kubembeleza mkuu wa chuo
Niko kawaida mmmwaaaah,alijibu judith na kumbusu sehemu ya kupitishia chakula mkuu wake huyu ambae kwasasa alikuwa ni mupeenzi wake mambo ya kielimu yaliwekwa kando.
Mkuu wa chuo alihisi kuchanganyikiwa akaanza kumtoa maganda yale aliyovaa na kumuacha kama ndizi iliyomenywa kisha nae akatoa maganda yote na kubaki kama judith wakaanza kunywa juisi za vinywa vyao hali hii ilimfanya judith kulegea kutokana na kutofanya muda mrefu lakini ghafla alikumbuka anamsaliti james aliacha akanyanyuka na kuanza kurudisha maganda yake ili yafiche utupu wake.
Kulikoni mama,aliuliza mkuu huyo
Siwezi nisamehe sana kiukweli nampenda sana mume wangu kamwe siwezi kumsaliti,alisema judith huku akimalizia kuvaa mavazi yake
Unasemaje wewe?,aliuliza mkuu huyo kwa ukali
Umenielewa nadhani akatoka na kumuacha kazubaa,alipanda lifti alipotua chini akapanda teksi mpaka chuo akapitiliza chumbani kwake akajilaza.
Hivi huyu binti ana matatizo gani au kashafanyiwa dawa?,alijiuliza mkuu huyo alinyanyuka akaingia bafuni akaoga akavaa mavazi yake alipomaliza akaondoka kuelekea kwake.
Itaendeleaaa

No comments:

Post a Comment